Kada wa CHADEMA Ole Sosopi amehojiwa na polisi leo Dar.soma zaid.
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Vijana wa Chadema Taifa(BAVICHA), Patric
Ole Sosopi leo amehojiwa Kituo Kikuu cha Polisi
Dar es Salaam kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu
inayotishia uvunjifu wa amani.
Sosopi alifika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi huku
ameambatana na wakili wake Frederick Kikwelo
huku wakisindikizwa na wafuasi watano wa
chama hicho.
Akizungumzia suala hilo baada ya kutoka polisi
mwanasheria wake alisema mwenyemkiti huyo
alihojiwa kwa nusu saa na alipewa dhamana na
jeshi la polisi huku wakiendelea na upelelezi wao
ambapo ukikamilika watakabidhi kwa mwendesha
mashtaka kwa ajili ya kupitia ushahidi.
Sosopi alisema baada ya kuhojiwa alielezwa na
jeshi la polisi kuwa arudi Julai 18 mwaka huu
lakini hawajampa sababu ya msingi ya kurudi
siku hiyo.
“Polisi hawajanipa sababu ya msingi ya kurudi
Julai 18 mwaka huu,”alisema Sosopi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu
alichohojiwa Sosopi, alisema hana taarifa hizo
hivyo atafuatiulia.chanzo mwananch.
0 comments :
Post a Comment