Lionel messi ahukumiwa kifungo chà miezi 21 jela.sima zaid.
Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel
Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela
baada ya kupatikana na makosa ya kutumia
ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya
habari nchini Uhispania vinaripoti.
Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa
kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m
(£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.
Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema
maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru
Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato
kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji
huyo.
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu
masuala yake ya kifedha.chanzo bbc Swahili.
0 comments :
Post a Comment