Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Kigamboni niyetu sote wana Dar es salaam tujitokeze kufanya usafi katika fukwe zetu 30/7/2016.soma zaid.

Balozi wa kujitolea katika kuhamasisha usafi wa
mazingira,
30.2016 anatarajia kuungana na wananchi
mbalimbali wa Kigamboni katika zoezi la
ufanyaji usafi katika fukwe ya Feri-Mnazi Kinda
mpaka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere Magogoni na jirani na Jeshi la Navy.
Kwa mujibu wa Balozi huyo, amebainisha kuwa
siku hiyo wananchi mbalimbali wameombwa
kujitokeza wakiwa na vifaa vyao vya kufanyia
usafi na kuungana kwa pamoja katika ufanyaji
wa usafi wa mazingira.
“Jumamosi ya Julai 30. Ni siku maalum ya usafi
wa mazingira yetu. Hivyo tutafanya usafi katika
fukwe za Feri kwani tayari fukwe hizi
zimeharibika vibaya kutokana na uchafu. Watu
wamegeuza bahari kuwa dampo, kitu ambacho
sio sahihi zoezi hili lina wahusu wadau wote
kutoka ndani ya Wilaya yetu mpya ya Kigamboni
na Mkoa kwa ujumla.” Alieleza Bwana Kombe.
Aidha, aliongeza kuwa, kuunga mkono juhudi za
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ya
kuhakikisha mazingira yanakuwa safi,
amewaomba wananachi kujitokeza kwa wingi
katika kushiriki zoezo hilo ambapo pia kutakuwa
na harambee yenye lengo la kukusanya fedha za
kujenga choo katika maeneo hayo ya Feri.
“Zoezi hili la usafi litakuwa ni kubwa na
endelevu. Pia kutakuwa na Harambee ya
kuchangisha fedha ambazo tutajenga Choo eneo
la feri. Kwa sasa hakuna choo na wavuvi na watu
wa maeneo yale kwani wamekuwa na tabia ya
baadhi yao kujisaidia pembeni mwa bahari kitu
ambacho sio sahihi kwani kinaweza kupelekea
magonjwa wa milipuko/maambukizi.
Tuungane kwa pamoja na Mkuu wetu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Bwana Paul Makonda, Meya
wa Jiji na wadau wengine mbalimbali kuliweka
jiji letu katika hali ya usafi” alimalizia Bwana
Kombe.
Mbali na tukio hilo la usafi. Pia Bwana Omary
Kombe anatarajia kutoa tuzo maalum ya
mazingira kwa Kamanda wa Jeshi la Navy,
kutokana na kujali kwao usafi wa Mazingira.
Balozi wa kujitolea katika kuhamasisha usafi wa
mazingira, Omary Kombe (kushoto) akitoa moja
ya vifaa vya usafi katika shughuli za
kuhamasisha usafi katika Jiji la Dar es Salaam.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top