Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Ufinyu wa bajeti wasababisha hospital ya moi kuzidiwa wagongwa.soma zaid

Dar es Salaam. Ufinyu wa bajeti katika Taasisi
ya Tiba ya Mifupa (MOI) umesababisha taasisi
hiyo kuzidiwa na wagonjwa wa upasuaji, huku
wengine wakisubiri huduma hiyo kwa zaidi ya
miezi minne.
Kabla ya tatizo hilo la kifedha MOI ilianzisha
kambi maalumu ya Jumamosi na Jumapili na
waliweza kuhudumia wagonjwa hadi 30 kwa
siku hizo mbili.
MOI kwa kawaida hutoa huduma ya upasuaji
kwa wagonjwa wanane hadi 10 kwa siku, lakini
kutokana na ufinyu wa bajeti uliosababisha
kuondolewa kambi za mwishoni mwa wiki,
umesababisha ongezeko la idadi kubwa ya
wagonjwa wanaohitaji upasuaji.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi katika
wodi ya MOI jengo jipya, umebaini uwapo wa
idadi kubwa ya wagonjwa waliokaa muda mrefu
wakisubiri huduma ya upasuaji, huku wengine
wakirejeshwa nyumbani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top