Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 2, 2016

Kiyama cha mafisadi na wahujumu uchumi kimefika.soma zaid.

, DAR ES SALAAM
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande
Othman, amesema ukarabati wa jengo la
mahakama maalumu kwa ajili ya kushughulikia
kesi za mafisadi utaanza Jumatatu.
Amesema mkandarasi aliyeteuliwa kukarabati
jengo hilo atakabidhiwa eneo la mradi ambalo ni
jengo la Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi, lililoko Chuo cha Sheria,
Ubungo, Dar es Salaam Jumatatu.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwasajili
mawakili wapya 623, iliyofanyika kwenye viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Jaji Othman
alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria
iliyopitishwa na Bunge.
“Muswada wa Sheria umeshapitishwa na Bunge,
hivyo karibuni utakwenda kwa Rais Dk. John
Magufuli kwa ajili ya kuusaini ili utangazwe kuwa
sheria katika gazeti la Serikali kabla ya kuanza
kutumika rasmi.
“Jumatatu mkandarasi atakabidhi jengo la
mahakama hiyo lililoko katika Chuo cha Sheria,
Ubungo ambapo kuna marekebisho yatafanyika
kabla ya kuanza kutumika,” alisema Jaji Othman.
Alisema mahakama ina wafanyakazi wa kutosha
kutenda shughuli zote za kimahakama na
imekwishateua majaji ambao watapewa semina
maalumu ya utendaji kazi katika mahakama ya
mafisadi.
Aidha, alisema usajili mpya wa mawakili 623
imeongeza idadi ya waliokuwepo hadi kufikia
5,800 na kwamba mawakili wapya waliosajiliwa
wanatoka sekta binafsi, serikalini, taasisi na
mashirika ya umma na walimu wa sheria katika
vyuo vikuu.chanzo mtanzania new paper.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top