Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 2, 2016

Wazir mwigulu nchemba awapa nasaha polisi kuwasaidia wananchi wanaoonewa.soma zaid.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba, jana alianza ziara yake ya kwanza
mkoani Dodoma tangu alipoteuliwa kushika
wadhifa huo kwa kutoa wito kwa Jeshi la Polisi
kuwasaidia wananchi wanaoonewa na wenye
nguvu.
Akizungumza na makamanda wa polisi wa wilaya
saba za Mkoa wa Dodoma, maofisa, wakaguzi na
askari wa kawaida, Waziri Mwigulu alisema
wananchi wanyonge wanaonewa na watu wenye
nguvu hivyo ni kazi ya jeshi hilo kuwasaidia ili
waweze kupata haki.
“Wapo watu wanaoonewa na wenye nguvu,
tuwasaidie ili yeyote anayeonewa aone uonevu
umekoma, tuwe ngao kwa wanaolia kwa
kuonewa,” alisema Waziri Mwigulu.
Aidha, waziri huyo alisema Jeshi la Polisi licha ya
kupambana na mtandao haramu wa wauzaji wa
dawa za kulevya linatakiwa kuongeza nguvu
katika mapambano hayo ili liweze kuufyeka
“Tukibaini mnyororo huo na kuukata kila
Mtanzania atajua uwepo wetu. Hakuna siku
tumewahi kuwa na mashaka na ninyi,
kinachotakiwa ni kuzingatia miiko ya kazi, fedha
za dili zinapopungua hata ukwapuaji wa hapa na
pale unaongezeka.
“Miongoni mwa matatizo nitakayoshughulika nayo
ni makazi ya askari, nitatafuta njia ya
kushughulikia tatizo hilo ikiwemo kutumia nguvu
mbadala,” alisema Waziri Mwigulu.
Waziri huyo pia alifanya ziara katika makazi ya
askari yaliyopo eneo la Barabara ya Iringa na
Nzuguni na kuahidi kuyaboresha pamoja na
kujenga mapya.
“Ingawa bajeti ni ndogo lakini nitahakikisha askari
wanakuwa na makazi mazuri na nitaanza na
maeneo ambayo hayahitaji fidia,” alisema Waziri
Mwigulu.
Aidha, waziri huyo alisema Serikali inakusudia
kujenga nyumba za mkoani Dodoma na aliwaasa
viongozi wa Serikali kutoa kipaumbele kwa
upatikanaji wa magari ya polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro
Mambosasa, aliyekuwa ameambatana na Waziri
Mwigulu katika ziara hiyo, alisema jeshi hilo
mkoani Dodoma litaendelea kufanya kazi kwa
weledi na kujituma ili kutimiza malengo ya
uwepo wake.chanzo mtanzania new paper

0 comments :

Post a Comment

Back To Top