Mwanasheria Takukuru atuhumiwa kwa kuomba rushwa.soma zaid.
MWANASHERIA wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa wilaya ya
Makete mkoani Njombe na mlinzi wa ofisi za
taasisi hiyo wilayani humo, wanashikiliwa na
Takukuru wakituhumiwa kuomba na kupokea
rushwa.
Watumishi hao wanatuhumiwa kuomba rushwa ya
Sh 600,000 kutoka kwa mtumishi
anayetuhumiwa kughushi vyeti vilivyomwezesha
kupata ajira.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe,
Charles Nakembetwa alimtaja mwanasheria huyo
kuwa ni Frednand Nsakuzi na Julius Hasani
ambaye ni mlinzi wa ofisi ya taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jana, Nakembetwa alisema watumishi hao
waliomba rushwa kwa mtumishi huyo ili kuficha
ukweli wa taarifa alizohusishwa nazo.
Alisema Takukuru kwa kushirikiana na mteja
wao huyo waliweka mtego uliofanikisha
kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kuongeza
kuwa mtego uliotegwa Juni 28, mwaka huu,
watuhumiwa hao walipokea Sh 100,000 kama
malipo ya awali katika tukio lililofanyika kati ya
saa 1:00 na 2:00 usiku.
“Walikamatwa wakati wakipokea kiasi hicho cha
fedha kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya
Mwaka 2007,” alisema. Alisema uchunguzi
unaendelea na ukikamilika watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani wakati wowote
kuanzia sasa.chanzo mtembezi.com
0 comments :
Post a Comment