Wàtu wanne wakamatwa kwa wizi wa umeme Arusha.soma zaid.
WATU wanane wamekamatwa jijini Arusha jana
baada ya kukutwa wakiiba umeme na
kulisababishia hasara Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania (Tanesco).
Akizungumza jijini Arusha jana wakati wa
operesheni ya kukamata wanaohujumu
miundombinu ya shirika hilo, Mdhibiti Mapato
wa Tanesco mkoa wa Arusha, Mhandisi Hassan
Juma Lumuli, alisema wizi wa umeme una
madhara makubwa na ndiyo maana hivi sasa
wanaendesha operesheni mbalimbali za
kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua za
kisheria.
Alisema wezi hao ambao hakuwa tayari
kuwataja majina yao kwa sasa, walikuwa
wakichezea mita ili wasomaji mita wa Tanesco
washindwe kusoma kiasi sahihi wanachodaiwa
na pia kujiunganishia kinyemela kwa kupitisha
nyaya chini ya ardhi.
Aidha, alisema mbali na kusababisha hasara
kutokana na wizi huo, pia madhara ya
kujiunganishia umeme kiholela ni mengi
ikiwamo vifo na upootevu wa mali baada ya
nyumba kuungua.
“Lakini tunachosikitika ni kuona kuwa baadhi ya
viongozi wa kidini na wa mitaa wakiwa sehemu
ya tatizo badala ya kuwa mfano mzuri kwa jamii
katika kufuata sheria na kuheshimu
miundombinu ya umeme ,” alisema
Akizungumzia suala hilo, Afisa Usalama wa
Tanesco mkoa wa Arusha, Kembe Sabini,
alisema kazi ya kukamata wezi wa umeme ni
endelevu na hivyo wengine wenye tabia hiyo
waache mara moja kwa sababu gharama za
umeme ni za chini na kwamba, wavunjao sheria
ni lazima watanaswa tu.
0 comments :
Post a Comment