Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 3, 2016

Vodacom yaendelea kuwajaza mamilioni washindi kupitia promotion yake.soma zaid.

Mkazi wa kitongoji cha Mkoani kilichopo
Nyamagana jijini Mwanza,Shomari Almas
ameibuka mshindi mwezi wa kitita cha
shilingi milioni 20 kupitia promosheni ya
”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na
Vodacom Tanzania.
Akiongea kwa furaha baada ya
kutangazwa kuwa ameibuka kuwa mshindi
wa droo ya mwezi Shomari Almasi ambaye
anajishughulisha na kilimo na ufugaji
alisema kuwa ndoto yake ya kuboresha
maisha yake imetimia.
“Nashukuru Vodacom kwa kuleta
promosheni hii kwa kuwa wakati nashiriki
sikujua kama nitaibuka na
ushindi.Nikipatiwa fedha hizo nitaendeleza
shughuli zangu za kilimo na ufugaji pia
mipango yangu ya kuoa na kuazisha
familia yangu itafanikiwa”.Alisema.
Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa
promosheni hii ambayo inaendelea
imeishawezesha wateja 61 wa Vodacom
kujishindia vitita vya mamilioni ya
fedha.Washindi 58 wamejinyakulia shilingi
milioni 1 kila mmoja,washindi watatu wa
mwezi wamejinyakulia shilingi milioni 5
kila mmoja.
“Napenda kutoa wito kwa wateja wetu na
watanzania wote kwa ujumla ambao
hawajajiunga na mtandao wetu waweze
kujiunga na kuchangamkia promosheni hii
kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi
Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila
mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/-
na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili
kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na
mwisho wa mwezi kuna mshindi wa
milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi
kubwa ya mwisho wa promosheni ni ya
kitita cha shilingi Milioni 100/= “Alisema
Aliongeza kusema kuwa ili mteja aweze
kushiriki katika promosheni hii ni rahisi
sana mteja anachotakiwa kufanya ni
kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa
kuandika neno “GO” kwenda namba 15544
ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha
kuwa ameingia kwenye mchezo na
ataanza kupokea maswali atakayotakiwa
kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za
ushindi na mteja atakatwa shilingi 300 tu
kwenye muda wake wa maongezi ”.
maswali atakayopokea mteja yatakuwa na
majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine
likiwa sio sahihi.
Kwa wateja ambao hawana nafasi ya
kujibu maswali ili wasipitwe na
promosheni hii alisema wanatakiwa
kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544
na atakatwa kiasi cha shilingi 200 tu
watakuwa hawahangaiki kujibu maswali
ila watakuwa wameingizwa kwa droo
moja kwa moja.
Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu (katikati)
akiongea na waandishi wa habari(hawapo
pichani)wakati wa kuchezesha droo ya
mwezi ya promosheni ya”Kamata
Mpunga”ambapo Shomari Almasi, mkazi
wa Mwanza,aliibuka mshindi wa mwezi
wa kitita cha shilingi Milioni 20/- Wengine
katika picha kushoto ni Ofisa msimamizi
wa michezo ya kubahatisha
Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa
huduma za ziada wa kampuni
hiyo,Mathew Kampambe.
Meneja Uendelezaji wa Masuala ya
Kibiashara wa Vodacom Tanzania
(Business continuity Management),Ajit
Mistry (kushoto) na Afisa msimamizi wa
michezo ya kubahatisha
Tanzania,Abdallah Hamed (wa pili
kushoto)wakimshuhudia Meneja Uhusiano
wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
(kulia)akiwaonyesha namba ya simu ya
Shomari Almasi mkazi wa Mwanza
aliyeibuka mshindi wa kitita cha shilingi
Milioni 20/- katika droo ya mwezi ya
promosheni ya ‘Kamata
Mpunga’inayowawezesha wateja wa
mtandao huo kujishindia pesa taslimu
kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla
ya washindi 61 wamepatikana kupitia
promosheni hiyo.Ili mteja aweze kushiriki
katika promosheni hii anatakiwa kutuma
neno “GO”kwenda namba 15544 aidha
mteja anaweza kujiunga moja kwa moja
kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba
15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu
maswali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top