Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, July 14, 2016

Kuwaiti imeahidi kuisaidia Tanzania sekta ya Afya.soma zaid.

Neema ya misaada kutoka kwa nchi marafiki
inataraji kuendelea kupokelewa nchini baada ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al- Najem.
Katika mazungumzo yao Balozi Al-Najem
ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati
ya Tanzania na Kuwait katika kusaidia sekta ya
Afya kwenye maeneo ya huduma ya Afya ya
mama na mtoto upande wa upatikanaji wa vifaa
vya kujifungulia(Delivery Kits) vitakavyotolewa
kwa wajawazito bila malipo.
Pia balozi Al-Najem aliongeza kuwa wataendelea
kusaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari kwa
kubadilishana wataalam kwa kipindi maalum.
Aidha Balozi huyo ameahidi kuisadia taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete ili kuboresha utoaji wa
huduma.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top