Maombi ya Tundu lissu wametupiliwa mbali mbali mahakamani kisutu Dar.soma zaid.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam imetupilia mbali maombi ya Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ya
kufutiwa mashitaka ya uchochezi yanayomkabili
na wenzake watatu.
Hakimu Mkazi Mkuu, Emillius Mchauru alitoa
uamuzi huo jana baada ya kukubali pingamizi
lililowasilishwa na upande wa Jamhuri waliodai
mashitaka hayo yasifutwe kwa kuwa hati ya
mashitaka haina makosa.
Mbali ya Lissu, washitakiwa wengine katika kesi
hiyo ni mwandishi wa gazeti la Mawio, Jabir
Idrissa, Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na
Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail
Mehboob. Hata hivyo, uamuzi huo ulitolewa jana
bila Lissu kufika mahakamani hapo kwa kuwa
anaumwa.
Akiieleza mahakama, Wakili wa utetezi, Peter
Kibatala alidai Lissu ameshindwa kufika
mahakamani kwa kuwa anaumwa, lakini
wadhamini wake akiwemo Ibrahim Ahmed
wamefika mahakamani na kueleza kuwa Lissu
anaumwa malaria. Aidha, ilielezwa kuwa
mshtakiwa Idrissa anaumwa na yupo Zanzibar
kwa ajili ya matibabu.
Katika maombi yao, washitakiwa kupitia kwa
Wakili Kibatala waliiomba mahakama ifute
mashitaka hayo kwa kuwa hati ya mashitaka
imekosewa kwa kutokueleza makosa hayo
wametenda wapi na pia mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza masuala yanayohusu
Zanzibar.
Akisoma uamuzi, Hakimu Simba alisema baada
ya mahakama kupitia hoja za pande zote mbili
katika kesi hiyo imejiridhisha kuwa hati ya
mashitaka haina makosa.
Aidha, alisema mahakama hiyo ina mamlaka ya
kusikiliza shauri hilo kwa kuwa makosa
yaliyofanyika yanahusu Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Hivi karibuni, mahakama ilifuta mashitaka
mawili ya uchochezi kati ya matano
yanayowakabili washitakiwa hao, baada ya
upande wa jamhuri kuyaondoa katika hati kwa
kuwa hayana kibali cha Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP).
Katika mashitaka yao inadaiwa Januari 12 hadi
14, 2016, Dar es Salaam washitakiwa
walichapisha taarifa ya uchochezi yenye kichwa
cha habari ‘ Machafuko yaja Zanzibar’.
Pia inadaiwa Januari 14, 2016 Dar es Salaam
walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa
wananchi wa Zanzibar. Inaendelea kudaiwa siku
hiyo hiyo, Lissu na wenzake bila ya kuwa na
mamlaka yoyote yale waliwatisha na kuwatia
hofu wananchi wa Zanzibar ili wasikubali kuingia
kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.
0 comments :
Post a Comment