Watu zaid 75 wamefariki dunia kutokana na mlipuko kutoka katika lori Ufaransa.soma zaid.
Wakati Wafaransa wakiwa katika Maadhimisho
ya Kitaifa ya Bastille, umetokea mlipuko katika
mji wa Nice kutoka katika lori na kusababisha
vifo vya wanaokadiliwa kufikia 80 na wengine
wakipata majeruhi kutokana na mlipuko huo
Taarifa kutoka Ufaransa zinaeleza kuwa lori hilo
lilifika katika eneo ambalo lina watu wengi na
kutokea mlipuko kisha baadae kulipatikana
bunduki na vifaa vingine vya ulipuaji katika lori
hilo.
Licha ya watu wanaokadiliwa kupoteza maisha
kutajwa kufikia 80, lakini pia idadi ya majeruhi
ambao wamepatikana katika tukio hilo
wanatajwa kuwa kufika 50.
Meya wa mji wa Nice, Christian Estrosi
amesema kuwa dereva wa lori hilo alipeleka gari
katika eneo ambalo lilikuwa na watu wengi kisha
kutokea mlipuko umeopelekea kutokea kwa vifo
hivyo na wengine kujeruhiwa.
Kutokana na tukio hilo, Rais wa Ufaransa
Francois Hollande ametangaza hali ya hatari
kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuimarisha hali
ya usalama na kusema kuwa Wafaransa kwa
sasa wapo katika vita na makundi ya kiislam
ambayo yamekuwa yakiwashambulia..
Hii inakuwa sio mara ya kwanza kutokea kwa
shambulio nchini Ufaransa kwani mwaka jana
mwezi Novemba kulitoke shambulio lingine
lililosababisha vifo vya watu 130.
0 comments :
Post a Comment