Sitta ameondolewa kwenyenyumba aliyokuwa akiishi masaki .soma zaid
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel
Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa
akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi
ya pango.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania,
mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika
nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na
kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake
tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.
Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge,
Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000
ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa
ajili ya nyumba hiyo.
Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika
Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi,
aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi
yake.
Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani
hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni
mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa
kuhamisha vitu kidogo kidogo.
“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa
tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui
kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila
sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese,
hapa hapa Masaki.
“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo
maana wanahama,” alisema.
Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari,
Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen
Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka
mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara
ya Fedha.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa
malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja
na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen
alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za
wastaafu kwa mujibu wa sheria.
“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio
wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki
zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria,
isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio
wahusika,” alisema.
Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki, alisema hana taarifa hizo za
kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.
Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake
ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi
kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza
kulisemea jambo hilo.
“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi,
halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.
Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili
kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:
“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu
unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo
vya habari.”
Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na
aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda,
ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia
matengenezo ya nyumba yake iliyoko
Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi
wake ulikumbana na lawama kali za wananchi
wanaoishi jirani na eneo hilo.
Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa
kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia
inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya
Sinza.
Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke
wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo,
alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye
nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe
alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la
Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo
walipaswa kuhama.
Chanzo: Mtanzania
0 comments :
Post a Comment