Mkuu wa wilaya ya kinondoni amefanya ziara hospital ya Tandale,uwanja wa fisi.soma zaid.
Akiwa na siku 85 tangu kuchaguliwa kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni April 21,
2016, Ally Salum Hapi ameendelea
kutekeleza kwa vitendo majukumu
aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Rais John Pombe
Magufuli.
Licha ya kusimamia suala la watumishi
hewa katika wilaya yake ambao walikuwa
34 na kufikia 101, huku akisimamia vyema
na Kulimaliza suala la upatikanaji wa
madawati katika wilaya yake ambapo
imekuwa changamoto kubwa tangu
kutangazwa kwa Elimu bure.
Mkuu wa Wilaya, Ally Salum Hapi
ameelendelea na kasi hiyo ya HAPA KAZI
TU ambapo leo ametembelea maeneo ya
Tandale Hospitali, Uwanja wa Fisi na Soko
la Tandale kwa ajili ya kusikiliza kero za
wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na wakazi hao amewataka
kuzingatia suala la usafi na kuhakikisha
wanakuwa na vifaa vya kuwekea uchafu
katika maeneo yao huku akiwasisitiza
wale wenye sehemu za kuegeshea magari
katika maeneo yao kuyaweka katika
mazingira ambayo hayataleta athari.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
akiwa na ujumbe wake, wakipita maeneo
ya Tandale Uwanja wa Fisi kwa ajili ya
kusikiliza kero za wakazi wa maeneo
hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
akizungumza na mmoja wa wananchi
wakazi wa Maeneo ya Tandale jijini Dar es
salaam leo.
0 comments :
Post a Comment