Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 23, 2016

Lori lavamia nyumba na kuua mwanafunzi mkoani lini.soma zaid.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya
sekondari Mnolela iliyopo katika halashauri ya
wilaya ya Lindi, Maulidi Yussuph miaka 16,
amefariki dunia papohapo baada ya gari aina ya
roli T 127 AGX, iliyokuwa imebeba mifuko ya
saruji ikitokea mkoani Mtwara kuelekea jijini Dar
es Salaam kuacha njia na kuingia ndani ya
nyumba alimokuwemo Maulidi pamoja na
familia yao wakila chakula.
Akizungumza na ITV eneo la tukio baba mzazi
wa marehemu, Yussuph Kalomba, amesema
jana majira ya saa kumi na moja jioni akiwa na
familia yake ya watu nane wakati wanakula
chakula sebureni, walisikia kishindo kikubwa nje
ya nyumba yao kilichoashiria kupasuka kwa tairi
ya gari huku kukiwa na sauti ya mburuziko
lakini kabla hawajajua hati yake gari hiyo
walistukia inabomoa nyumba waliyokuwemo na
kuingia mpaka ndani hali iliyosababisha taharuki
ndani ya nyumba hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha
Zingatia, kata ya Mnolela, halmashauri ya
wilaya ya Lindi, Salumu Zalafi, amesema eneo
hilo limekuwa likitokea ajali za mara kwa mara
kutokana na kona kali iliyopo sehemu hiyo hali
inayotishia maisha ya wakazi wanaoishi maeneo
hayo huku wakiiomba serikali kuwawekea
matuta ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa
zikitokea mara kwa mara.
Marehemu Maulidi Yussuph amezikwa leo
asubuhi majira ya saa nne katika kijiji cha
Zingatia, kata ya Mnolela, halmashauri ya
wilaya ya Lindi.
ITV ilimpigia simu kamanda wa polisi mkoa wa
Lindi, Ranata Mzinga ili kuthibitisha kutoke ajali
hiyo pamoja na kifo cha mwanafunzi Maulidi
Yussuph lakini simu yake haikupatikana
kutokana na kamanda huyo kuwa nje ya Lindi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top