Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 23, 2016

Mo Dewji kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii masikini.soma zaid.

KURUGENZI Mtendaji wa makampuni ya
Mohammed Enterprises Tanzania Limited
(METL Group), Mohammed Dewji, ameungana
na matajiri wakubwa duniani, kutangaza azma
ya kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii.
Taarifa kutoka mtandao mashuhuri duniani wa
Forbes, imesema kuwa Dewji, ambaye ni
bilionea kijana kuliko wote barani Afrika,
ameingia katika kundi la matajiri hao ambao
wametoa ahadi ya kutoa nusu ya mali zao,
kusaidia jamii.
“Baada ya kushuhudia umasikini mkali wakati
nikilelewa, siku zote nimekuwa nikijisikia
kuwajibika kutoa kwa ajili ya jamii yangu,”
amesema Dewji katika barua yake ya kutangaza
ahadi hiyo, ambayo ameiweka wazi kwa
waandishi wa habari.
Alishukuru wazazi wake kwa kumuunga mkono
na kumjengea moyo wa kusaidia jamii na
kipekee katika wajibu wake kwa dini yake ya
Uislamu wa kutoa na kujali wahitaji na jamii.
Bilionea huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza
kuungana na matajiri duniani, Bill Gates na
Warren Buffett katika kutangaza nia hiyo tangu
2010 na kushauri watu wengine wenye uwezo
kujitolea kwa ajili ya jamii.
Kundi la matajiri waliokwisha kutangaza nia hiyo
ya kutoa sehemu ya mali zao kwa jamii,
limeshafikia 155 kutoka nchi 17, ambapo Juni
mwaka huu, kundi hilo linalotambuliwa kwa jina
The Giving Pledge, lilitangaza kupata wajumbe
wapya 17.
Wajumbe wa mwanzo wa kundi hilo ni pamoja
na Eli Broad na mkewe Edythe, John Doerr na
mkewe Ann pamoja na mmoja wa wamiliki wa
Facebook, Mark Zuckerberg na mkewe, Priscilla
Chan.
Mtandao mashuhuri wa Forbes, umemkadiria
Dewji kuwa anamiliki mali zenye thamani ya
Dola za Marekani bilioni 1.1, akiongoza kundi la
makampuni ya METL nchini Tanzania,
linalojihusisha na biashara za viwanda vya
nguo, vinu vya unga na viwanda vya mafuta ya
kula, huku kinywaji chake cha Mo Cola, kikiuzwa
bei rahisi kuliko kununua Coca-Cola.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top