Bodi ya mikopo kutangaza majina ya wale ambao hawajajitokeza kurejesha mikopo.soma zaid.
Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku
60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza
kurejesha mikopo yao.
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri
kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato
ya marejesho. Baada ya kipindi hicho
kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa
ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu
wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia
wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale
wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza
kurejesha mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao
hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.
Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa
kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu
cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa
kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha
taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za
Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao
kabla ya zoezi la kutangaza majina
halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika
kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka
usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua
zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
0 comments :
Post a Comment