Breaking News
Loading...

Advert

Friday, July 22, 2016

Kamati kuu CHADEMA kukutana kwa dharura leo Dar se salaam.soma zaid.

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa dharura,
jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa
Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja
na masuala mengine, itapokea taarifa na kujadili
hali ya siasa nchini.
Katika siku za hivi karibuni, taifa limekuwa
likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa ni
pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria na
taratibu za kuongoza nchi unaofanywa waziwazi
na mamlaka za juu/viongozi waandamizi wa
nchi kupitia kauli na matendo mbalimbali kiasi
cha kuwashtua Watanzania ambao wangependa
kuona nchi yao ikiendeshwa katika misingi ya
uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24,
mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na
kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu
mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga
chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa
ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha
misingi kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima,
kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.
Imetolewa Ijumaa, Julai 22, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA

0 comments :

Post a Comment

Back To Top