Msichana afariki dunia baada ya kumchomwa sindano ya kutoa ujauzito.soma zaid.
Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Mwanza
imeeleza kwamba tarehe 20.07.2016 majira ya
saa 2:00 asubuhi katika kijiji cha Nyamatara kata
ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza,
msichana aliyejulikana kwa jina la Anna Martine
miaka [18] makazi kijiji cha Matara, alifariki
dunia.
Msichana huyo alifariki baada ya kuchomwa
sindano ya kutoa ujauzito wa miezi 03 na
muuzaji wa duka la dawa baridi wa hapo kijijini
kwao aliyejulikana kwa jina la Stephen Ng’wanyi.
Inadaiwa kuwa tarehe 19.07.2016 siku ya
Jumanne marehemu alikuwa akilalamika kuumwa
na tumbo kwa siku nzima, na ilipofikaJumatano
ya tarehe 20.07.2016 maumivu ya tumbo yalizidi,
ndipo alipoamua kumweleza ukweli dada yake
anayeishi naye aitwaye Anna Fabian kuwa ana
ujauzito wa miezi 03 na amechomwa sindano ya
kutoa ujauzito na Stephen Ng’wanyi.
Aidha inadaiwa kuwa baada ya hali ya marehemu
kuzidi kuwa mbaya, dada wa marehemu Bi Anna
Fabian aliamua kwenda kumwita bwana Stephen
Ng’wanyi ili aweze kuja nyumbani kwao na
kumpatia matibabu mdogo wake.
Bwana Stephen alipofika aliwaomba ndugu zake
aondoke na mgonjwa ili akampatie matibabu
nyumbani kwake, na baada ya dakika kadhaa
alirudi na kuwaeleza ndugu zake kwamba
mgonjwa amefariki dunia na baada ya kutoa
taarifa alitoroka kusiko julikana.
Jeshi la polisi lipo katika msako wa kuhakikisha
mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika katika kifo
hicho anatiwa nguvuni, huku uchunguzi pamoja
na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ukiwa bado
unaendelea.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya
wilaya ya Magu kwa ajili ya uchunguzi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
ACP Augustino Senga anatoa wito kwa wananchi
hasa wasichana kwamba kutoa mimba bila
sababu za kitabibu ni kosa la jinai na kuwashauri
kutofanya hivyo.
Aidha wamiliki wa maduka ya dawa baridi
wafanye biashara hiyo kwa mujibu wa leseni na
taaluma zao na sio vinginevyo.
0 comments :
Post a Comment