Maafisa Afya kortin kwa kutelekeza uchafu kahama.
MKUU wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu
amewatia mbaroni maofisa afya wa halmashauri
ya mji wa Kahama kwa tuhuma za kuacha
uchafu katika barabara kuu ya mji wa Kahama ya
kwenda katika nchini za jirani za Rwanda na
Burundi zikitoa harufu mbaya.
Maofisa walioswekwa ndani ni Johanes
Mwebesya na mtendaji wa kata ya Nyasumbi
Enocent Kapeli wanaotuhumiwa kuacha wananchi
wakitupa taka katika eneo lisilostahili eneo
lililopo mwanzo mwa barabara kuu ya kuingia
katika mji wa Kahama eneo la Phatom.
Awali mkuu huyo wa wilaya alipita eneo la
phatom akielekea halmashauri ya Ushetu kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya kawaida ndipo aliona
rundo la uchafu katika barabara hiyo kuu ya
kuingia Kahama Mjini, jambo ambalo alieleza
linaleta sura mbaya kwa mji wa Kahama.
Alitoa maagizo kabla ya kuondoka kwenda
Halmashauri ya Ushetu mbele ya Mkurungezi wa
Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson
Msumba pamoja na Mtendaji wa kata hiyo na
Ofisa Afya wa kata hiyo kuwa akirudi kutoka
Ushetu akute uchafu huo umeondolewa hapo
haraka jambo ambalo halikutekelezeka.
0 comments :
Post a Comment