Oscar pistorius ahukumiwa jela kifungo cha miaka 6.soma zaid.
Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika
Kusini Oscar Pistorius leo amehukumiwa kifungo
cha miaka sita jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi
wake Reeva Steenkamp .
Kesi ya Mwanariadha huyo iliendelea kwenye
mahakama kuu nchini humo na hukumu kutolewa
muda mfupi uliopita.
Awali Pistorius alikuwa anakabiliwa na kifungo
cha miaka 15 jela baada ya vita ya kisheria
iliyochukua takriban miaka mitatu.
Mwanariadha huyo Oscar Pistorius tayari
ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa
jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na
hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.
0 comments :
Post a Comment