Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 6, 2016

Donard Trump amemsifu saddam hussein.soma zaid.

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa
zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema
aliweza kukabiliana vyema na magaidi.
Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa
kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne
alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo
aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.
“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini
mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya
vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo
vyema sana,” Trump alisema.
“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote.
Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.”
Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na
Saddam
Trump: Ninaweza kuzungumza na Kim Jong-
un
Bw Trump awali amewahi kusema kwamba
ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko
sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam
Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya
Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.
Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani,
ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq
ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya
Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.
Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu
sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa
kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa
viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”
Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni
jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa
Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai
kuhudumu kama rais.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top