Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Rais Obama ampigia Debe mgombea urais Hillary Clinton Marekani.soma zaid.

Rais wa Marekani Barack Obama amemsifu sana
mgombea wa chama cha Democratic Hillary
Clinton na kusema ndiye afaaye zaidi kuongoza
Marekani.
Akihutubu katika kongamano kuu la chama cha
Democratic mjini Philadelphia, huku akishangiliwa
na wajumbe, Rais Obama amesema hakujawahi
kuwa na mtu aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani
kuliko Bi Clinton.
"Hakujawahi kuwa na mwanamume au
mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu
mwingine yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa
rais kama yeye," amesema Bw Obama.
Amemsifu pia kwa kujikakamua na kuwa
mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa
hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama
kikubwa.
Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda
nafasi zaidi kwa Wamarekani.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton
anatetea umoja na maadili ya Wamarekani.
Sababu ya nduguye Obama kumuunga mkono
Trump
Bill Clinton: "Rafiki yangu" Hillary anafaa
kuwa rais
Bw Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa
chama cha Republican Donald Trump.
Awali, Seneta wa Virginia Tim Kaine alikubali rais
uteuzi wa kuwa mgombea mwenza wa Bi
Clinton.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top