Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Watumishi 4 idara ya Afya Hospital ya Sinza Palestina wasimamishwa kazi.soma zaid.


WATUMISHI wanne wa Idara ya Afya, akiwemo
daktari mmoja wa Hospitali ya Sinza Palestina,
Alphonce Chiwambo wamefukuzwa kazi baada ya
kuthibitika kuwa na makosa ya rushwa na utoro
kazini.
Pamoja na kufukuzwa kazi kwa watumishi hao,
daktari mwingine wa hospitali hiyo amepewa
onyo baada ya kubainika kuwatoza wagonjwa
vitu mbalimbali vya matibabu ikiwemo pamba.
Watumishi hao wanne waliofukuzwa kazi, ni
miongoni mwa watumishi wanane wa Idara ya
Afya waliofunguliwa mashauri ya nidhamu.
Katika hatua nyingine, watumishi watatu kati ya
tisa wa Idara ya Uhandisi ambao pia walikuwa
wakichunguzwa wamethibitika kuwa na hatia na
kwa mujibu wa kanuni za utumishi wamepewa
adhabu mbalimbali.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace
Jacob aliyasema hayo jana na kuwataka
watumishi wanne waliosimamishwa kuwa ni
Athuman Hassan ambaye ni Ofisa Afya wa
Mazingira, Martin Malugu (Mteknolojia Msaidizi),
Abdulla Ussi (Mteknolojia wa Dawa) na Alphonce
Chiwango ambaye ni Ofisa Muuguzi Msaidizi wa
Hospitali ya Palestina.
Kwa mujibu wa Jacob, hatua hiyo imekuja baada
ya Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo katika
mkutano wake maalumu wa mashauri ya
nidhamu uliofanyika Julai 26, mwaka huu, pamoja
na mambo mengine ulitoa maamuzi kwa
watumishi 18 kufunguliwa mashauri hayo.
Alisema mashauri hayo yalikuwa ni dhidi ya
watumishi tisa wa Idara ya Uhandisi, watumishi
wanane wa Idara ya Afya na mtumishi mmoja wa
Idara ya Fedha na Biashara.
Alisema kwa upande wa wahandisi, wawili
wameshushwa vyeo na madaraja huku mmoja
akishushwa daraja na kupewa onyo na mtumishi
mwingine wa Idara ya Fedha na Biashara
amepewa onyo kali.
“Uamuzi wa baraza wa kuwapa onyo kali,
kuwashusha madaraja na kuwashusha vyeo
unatokana na ukweli kuwa walishindwa kutumia
taaluma yao vizuri kushauri njia nzuri ya kufanya
maamuzi ya mabadiliko ya ujenzi wa barabara za
Biafra, Journalism Phase II na Barabara ya
Maandazi,” alisema Meya Jacob.
Aliongeza kuwa baraza hilo limezingatia taratibu
zote katika kuchukuwa hatua za kinidhamu dhidi
ya watumishi hao, ikiwa ni pamoja na kufanyika
kwa uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma na
kufungua mashitaka dhidi yao.
Aliagiza watumishi sita waliothibitika kuwa
hawana makosa warejee kazini na kuendelea na
majukumu mengine. Akielezea sakata la daktari
wa Hospitali ya Sinza Palestina, Meya huyo
alisema kuwa daktari huyo aliomba rushwa ya Sh
300,000 ili kumfanyia upasuaji mjamzito ambaye
alimpatia Sh 250,000 pekee .
Alisema mama huyo alimuahidi Chiwambo
kwamba atampatia fedha iliyobaki baada ya
kupona, lakini baadaye aliamua kutoa taarifa
kuhusu tuhuma hiyo, na kuwezesha daktari huyo
kukamatwa.chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top