Breaking News
Loading...

Advert

Friday, July 29, 2016

RC Makala ameongea na wananchi wa mbeya kama utaratibu wake wa kila Alhamis mwanzo mwa mwezi na mwisho mwa mwezi.soma zaid

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla
ameendelea na utaratibu aliojiwekea wa
kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia
ufumbuzi kila siku ya Alhamisi ya mwanzo
wa mwezi na siku ya alhamis ya mwisho
wa mwezi, kama kawaida siku ya leo
mamia ya wananchi wamejitokeza Mbele
ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha kero zao.
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa
wilaya na watendaji wa ngazi zote
kuwasikiliza wananchi na kutatua Kero
zao "Kero Nyingi hapa ni za Halmashauri,
Wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu
wa Idara tafadhalini hakuna jambo kubwa
katika Uongozi kama kuwa Karibu na
unaowaongoza, kuwa msikivu na
kushughulikia matatizo yao kwa umati
huu ni dhahiri hamjatimiza majukumu
yenu na kwa kuwa MaDc, ma Ded ni
wapya sasa anzeni kazi hii kwa kasi "
Amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha
upelelezi wa kesi na pia kuepuka vitendo
vinavyolalamikiwa kwa baadhi ya Askari
kubambikizia Wananchi kesi
Amehaidi kuendeleza utaratibu huu kwa
muda wote mpaka siku atakapofika
ukumbini akute hakuna Mwananchi
aliyeleta Kero.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos
Makalla akiendelea kuratibu na Kuandika
baadhi ya kero Sanjari na Afisa Tawala
wa Mkoa wa Mbeya Mh.Mariam Mtunguja
katika ukumbi Mdogo uliopo Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Jijini Mbeya.
Kutoka Shoto ni Mkuu wa Wilaya Ya
Mbeya Mjini mh,William Mtimika, Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla
na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mbeya
Mh.Mariam Mtunguja Wakiendelea na
kazi ya kunukuu kero za wananchi walio
hudhuria kuwasilisha kero zao (Hawapo
Pichani).
Baadhi ya Wananchi wa wakitoa Kero Zao
mbele ya Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya
Mh.Amos Makalla.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top