Jumla ya wanafunzi 69,820 wameomba mikopo kwa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu.(HESLB).soma zaid
JUMLA ya wanafunzi 69,820 wameomba mikopo
kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) hadi sasa ikiwa zimebaki siku tatu
kufikia mwisho wa kupokea maombi hayo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam ,
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano
wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisoga, alisema
mwaka jana walioomba kupewa mikopo
walikuwa 65,000, hivyo waombaji wa mwaka
huu wameongezeka.
Mwaisoga alisema tofauti na awali, mchakato
wa sasa wa kuomba unafanyika kwa njia ya
mtandao na baada ya kutumwa kwao,
watayapitia na kwa yale yenye kasoro, wahusika
wataitwa ili wayarekebishe.
Alisema dirisha la uombaji wa mikopo linatarajia
kufungwa Jumapili hii.
Katika hatua nyingine, alisema idadi ya
wanaorejesha mikopo imeongezeka maradufu
baada ya kutakiwa kufanya hivyo.
“Kwa sasa ni vigumu kutaja idadi yao kwa sababu
huwa tunaitoa mwishoni mwa mwezi kwa hiyo
kesho tutakuwa na idadi kamili ya waliorejesha,
lakini ikilinganishwa na huko nyuma, sasa hivi
mwitiko wa wanaorejesha umeongezeka,”
alisema.
Mwaisoga alisema sheria inamtaka aliyekopa
aanze kurejesha baada ya mwaka mmoja wa
kuhitimu masomo yake, lakini
anapochelewesha, kila mwaka kunakuwa na
penati ya ongezeko la asilimia sita.chanzo mpekuzi blog
0 comments :
Post a Comment