Serikal imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo.soma Zaid.
Kwakifupi ni kwamba Serikali imezuia
Benki kupandisha viwango vya tozo katika
miamala yake na kuelekeza gharama hizo
kwa wateja wao.
Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata
amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya
iliyopitishwa kwenye miamala ya benki
inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa
na benki hizo kwa wateja wao lakini
serikali ilikuwa haipati chochote.
Kidata amesema kuwa Benki Kuu
imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa
kufanya ujanja wa kuongeza makato
kwenye miamala ya wateja wao wakati
wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi
hiyo mpya.
Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi
kinachotozwa kwenye miamala hiyo
kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini
serikali itakata kodi yake ya asilimia 18
na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa
sheria.
UPDATES:
Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA'
imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya
ongezeko la thamani kwenye huduma za
kifedha kuwa marekebisho ya sheria ya
mwaka 2014 yaliyopitishwa na bunge
yanayolenga kutoza kodi la ongezeko la
thamani kwa kiwango cha 18% kwenye
ada ambazo benki inatoza wateja wake
kwenye huduma mbalimbali zitolewazo na
benki au taasisi za fedha.
TRA wamesema taasisi za fedha
wanapoongeza makato ya miamala ya
fedha wanakosea kwa kupandishia
wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu
fedha ambayo mwanachi alikuwa
anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo
mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo
hizo ndizo zitakazokatwa 18%.
Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000
na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi
lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio
itakatwa 18% na sio mwananchi
kuongezewa makato kama ilivyofanyika
kwa baadhi ya taasisi za fedha.chanzo jamii forums.
0 comments :
Post a Comment