January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Tbs limetoa ovyo kali kwa watu wanaozalisha mafuta ya vilainishi vya mitambo na magari.soma zaid

Dar es Salaam.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS)
limetoa onyo kali kwa watu wanaozalisha
mafuta ya vilainishi vya mitambo na
magari visivyo kidhi viwango vya kitaifa
na kimataifa, kuwa watachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,
Dkt. Egid Mubofu (Pichani)amewaambia
waandishi wa habari jana jijini hapa kuwa
shirika hilo halitakuwa na mjadala kwa
wale watakaobainika na kuwaonya
waache mara moja.
“Hivi karibuni shirika lilifanya msako
mkali wa mafuta ya vilainishi vya
mitambo na magari visivyo na viwango na
kufanikiwa kuyabaini katika wilaya za
Temeke na Ilala,” alisema Dkt. Mubofu.
Alisema katika msako huo walikikamata
kiwanda bubu wilayani Temeke na
kukifungia na kwamba sheria itachukua
mkondo wake.
Katika msako huo lita 12,296 za vilainishi
vya injini zilikamatwa, lita 811 za
vilainishi vya mifumo ya breki na
kilainishi aina ya ATF lita 1,241; jumla
vikiwa na thamani ya Tshs milioni 46.
Pia aliwataka wazalishaji na waagizaji wa
bidhaa kutoka nje ya nchi kuwapatia
bidhaa bora watanzania.
Dkt. Mubofu aliwataka wananchi kususia
bidhaa isiyo na alama ya ubora ya TBS
kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
“Bidhaa za vilainishi na bidhaa nyingine
zote zinapoingizwa nchini lazima
zikaguliwe kwa kufuata viwango
vinavyotakiwa,” alisema.
Alisistiza kuwa mtu yoyote anayezalisha
au anayetaka kuzalisha ni lazima afuate
taratibu za nchi.
Alisema shirika litaendelea kufanya kazi
kwa kushirikiana kwa karibu na vyombo
vingine nchini kama Jeshi la Polisi na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
miongoni mwa vingine katika kudhibiti
bidhaa zisizo na viwango.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Shirika
linategemea sana ushirikiano wa
wananchi katika kupata taarifa na
kuwataka wanaoishi mipakani kuendelea
kutoa taarifa pale wanapoona bidhaa
zinapita bila kufuata taratibu ili kubaini
bidhaa hafifu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top