Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Mbunge amepiga Marufuku kucheza bao mida ya kazi.


MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah
Ulega amewataka vijana wa Wilaya hiyo
kujiunga katika vikundi vya vikoba
vinavyoazishwa kwenye maeneo yao na
kwamba wastarajie kuwa ahadi ya rais ya
kutoa sh. Milioni50 kila kijijihaitaenda
kwa mtu mmoja mmoja bali kwa kukaa
katika makundi.
Amesema kuwa kama wananchi wanataka
fedha hizo ziwafikie lazima wakae kwenye
vikundi na si vinginevyo ,huku akisisitiza
akina baba nao kuacha kutumia muda
wao mwingi kucheza bao badala yake
wajiunge katika vikundi.
Ulega ametoa wito huo jimbo humo
wakati akizungumza na wanachama wa
kikundi cha Vikoba cha Tuamke kilichopo
katika kijiji cha Lupondo kata ya mkamba.
Alisema kuwa hakuna namna kwani
maendeleo yanakuja Kwa kukaa katika
vikundi mbalimbali na hata fedha za rais
zitaelekezwa katika vikundi hivyo,hivyo
kazima watanzania wachangamkie fursa
hiyo.
"Binafsi Leo nawachangia sh.laki tatu
kwani mmeonesha dhamira ya dhati
kupitia risala yenu ambayo mmesoma
mbele yangu nami nahaidi nitakuwa
pamoja nami kamwe si tawaacha."alisema
Ulega.
Aidha alisema kuwa yeye kama mbunge
kuna mipango mingi ambayo anayo Kwa
ajili ya watu wake ikiwa pamoja na kuleta
watu wenye makampuni ya Pikipiki ili kuja
katika wilaya hiyo na kukopesha vijana
Pikipiki hizo na baadae kulipa
kidogokidogo Kwa muda wa miezi 11.
Alisema kuwa lazima vijana,akina baba
na akina mama Kwa pamoja wakubali
kutengeneza vikundi vya vikoba kwani
fursa nyingi zinapitia katika vikoba na si
Kwa mtu mmoja mmoja.
Aidha Ulega akiwa katika ziara ya kijiji
cha Lupondo alipata fursa ya kufungua
jengo la Tuamke Vikoba ambapo pia
alitembelea Zahanati ya Kijiji hicho
nakuhaidi kutatua tatizo la miundombinu
ya Maji.
Alisema kuwa anatambua kuwa Zahanati
hiyo inachangamoto kubwa ya Maji hivyo
atahakaikisha anasimamia ujenzi wa
kisima pamoja na kuona Zahanati hiyo
inapata umeme wa Tanesco Kwa ajili ya
kurahisisha utoaji huduma.
"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu wote
kuleta umeme hapa na kama ule wa
tanesco utachelewa basi nitahakikisha
naleta solar hapa."alisema Ulega.
Pia mbunge huyo alisema kuwa wananchi
watambue kuwa yupo Kwa ajili yao na
kwamba watakuwa pamoja katika kipindi
chonde cha uongozi wake ikiwa pamoja na
kuhakikisha anasukuma huduma jwa
wananchi wake.
Naye Diwani wa Kata Dundani ,Hassan
Dunda aliwaeleza wananchi hao kuwa
uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi
huku akisisitiza kuwa watu kukaa katika
makundi Kwa ajili kupata mikopo.
Ulega mbali na kufanya ziara katika kijiji
cha Kupondo pia alitembelea vijiji vingine
mbalimbali ndani ya Kata ya Mkamba
,ambapo pia anaendelea na ziara hizo za
kutoa shukrani na kukagua miradi ya
maendeleo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top