TFF yatangaza nafasi ya ajira idara ya masoko.soma zaid.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limeongeza muda zaidi kuimarisha idara zake
ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa
Watanzania wenye sifa za Idara ya Masoko na
Habari ili kuongoza Idara hiyo.
Awali tarehe ya mwisho ilikuwa Julai 11, 2016
lakini kwa sasa tarehe ya mwisho itakuwa Julai
19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF
imetangaza ajira.
Lengo hasa ni kuendana na hali halisi ya
uendeshaji mpira wa miguu duniani ambako
masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa
yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili
ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu
popote duniani.
Pili ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha
mpira wa miguu zinatokana na soka na vilevile
kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa
wakati mwafaka.
Kwa nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao
www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo
kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz
Mbali ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko,
pia TFF imepania kutoa kipaumbele katika
masuala ya waamuzi na wanawake kwa
kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi
ya Ufundi. Hapo awali madawati ya wanawake
na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa
kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).
Akizungumza na www.tff.or.tz, Katibu Mkuu wa
TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto
mbalimbali za soka la wanawake miongoni
mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji,
Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma
mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa
bidhaaa (products) za soka la wanawake.
Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo
hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa
katika kupata waamuzi wenye viwango vya
Kimataifa.chanzo dewji blog
0 comments :
Post a Comment