Wananchi wa pangani wakabilia kupata neema ya usafiri soma zaid.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi. Lekujan
Manase pamoja na Wakurugenzi kutoka
Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme
iliyo katika Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Dkt. William
Nshama pamoja na Mhandisi Lazaro
Vazuri wametembelea na kukagua mradi
wa ujenzi wa kivuko kipya cha Pangani,
pamoja na ukarabati wa kivuko cha
magogoni katika eneo la bandari ya Dar
es Salaam.
Wakikagua Mradi wa Ujenzi wa Kivuko
kipya cha Pangani Mhandisi Lekujan
Manase alisema; “Kivuko hiki kipo katika
hatua za mwisho za ujenzi wake na leo
tumekuja hapa kukagua mitambo ya
kuendeshea kivuko (propulsion units)
pamoja na engines zilizofungwa katika
kivuko hiki ili kukamilisha ujenzi wake na
hatimae kianze kufanya kazi”.
Mkandarasi Mkuu kutoka Songoro Marine
Transport LTD (ambao ndio wajenzi wa
kivuko hicho), alisema ujenzi wa kivuko
hicho unatarajia kukamilika mwishoni
mwa mwezi huu wa saba na kwamba
kivuko hicho kina uwezo wa kubeba
magari sita na abiria 100 kwa pamoja,
sawa na tani 50.
Nae Mhandisi Dkt. William Nshama
alieleza kuwa ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wa kivuko hicho unaofanywa kwa
kiwango cha kimataifa na kuwa kivuko
cha Pangani kinatarajiwa kutoa huduma
kati ya Pangani na Bweni Mkoani Tanga
baada ya ujenzi wake kukamilika.
Katika hatua nyingine Mtendaji Mkuu
TEMESA na ujumbe wake wamekagua
ukarabati wa kivuko cha Magogoni,
ambao uko katika hatua za mwisho za
ukarabati wake, kwani kwa sasa tayari
mitambo ya kuendeshea kivuko pamoja na
“engines” zinafungwa pamoja na
kumalizia matengenezo ya milango yaani
“ramps”. Ukarabati wa kivuko cha
magogoni unatarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwezi huu wa saba.
Kivuko cha Magogoni kinatoa huduma kati
ya Magogoni na Kigamboni, Dar es
Salaam.
Wakikagua mtambo wa kuendeshea kivuko
(propulsion unit), kutoka Kushoto ni
Mhandisi Lekujan Manase (Mtendaji Mkuu
TEMESA), Major Songoro ( Mkurugenzi
kutoka Songoro Marine Transport Ltd),
Vitus Bujimu (Mwakilishi Kutoka Songoro
Marine Transport Ltd), Mhandisi Lazaro
Vazuri ( Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Idara ya
Huduma za Ufundi na Umeme), Mhandisi
Japhet Maselle ( Mkurugenzi wa Huduma
za Vivuko kutoka, TEMESA) pamoja na
Mhandisi Dkt. William Nshama
(Mkurugenzi,Wizara ya Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano, Idara ya Huduma za
Ufundi na Umeme).
Kivuko kipya cha pangani katika hatua za
kukamilishwa kwa ujenzi wake,
unaofanyika katika eneo la bandari ya
Dar es salaam.
Kivuko cha Magogoni katika hatua za
kukamilishwa ukarabati wake. Kivuko hiki
kinatoa huduma kati ya Magogoni na
Kigamboni, Mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya juu ya Mlango wa kivuko cha
Magogoni.
Sehemu ya chini ya mlango wa Kivuko cha
Magogoni inayokuwa kwenye maji wakati
wa uendeshaji wa kivuko. Kutoka kulia ni
Major Songoro ( Mkurugenzi kutoka
kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd
inayokarabati kivuko hicho) akimuelezea
jambo Mhandisi Dkt. William Nshama
(Mkurugenzi Wizara ya Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano, Idara ya Huduma za
Ufundi na Umeme) alie chuchumaa ni
Mhandisi Japhet Maselle (Mkurugenzi wa
Huduma za Vivuko kutoka TEMESA).
MICHUZI BLOG at Wednesday, July 1
0 comments :
Post a Comment