Wananchi wa nyamungu waipinga serikali kuhusu utafiti.soma zaid.
Wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka
mgodi wa Dhahabu wa North Mara wilayani
Tarime mkoani Mara, wameshindwa kukubaliana
na matokeo ya uchunguzi wa serikali kuhusu
vipimo vya maji yanatiririshwa na mgodi huo
ambayo yanadaiwa kusababisha madhara
makubwa kwa binadamu, mifugo na mimea.
Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa
taarifa hiyo ya uchunguzi mbele ya waziri wa
nishati na madini Mh Prof Sospeter Muhongo,
wananchi hao wakiongozwa na mbunge wa
jimbo la Tarime Mh John Heche, wamesema
wanasikitishwa na taarifa hiyo kuonesha kuwa
maji hayo ni salama wakati bado kuna idadi
kubwa ya wananchi wakiwemo watoto ambao
wameathirika na maji hayo.
Awali akiwasilisha taarifa ya uchunguzi huo,
mkaguzi mazingira kutoka baraza la taifa la
hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC Bw
Peres Joshua, amesema uchunguzi huo
umebaini kuwa maji yanatiririshwa na mgodi
huo na kuingia katika mto Tigete ni salama na
kwamba hayana madhara yoyote kwa binadamu
na mifugo.
Hata hivyo waziri huyo wa nishati na madini Mh
Prof Sospeter Muhongo, akizungumza baada ya
kuwasilishwa kwa taarifa hiyo ya uchunguzi,
ameshauri uchunguzi huo ufanyike upya kwa
kuhusisha idara mbalimbali, huku akitoa ahadi
ya kupeleka sapuli ya maji hayo katika nchi tano
duniani ili kupata vipimo vilivyo sahihi ili
kuondoa utata huo.
0 comments :
Post a Comment