Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, July 19, 2016

Mahakama imetoa hati ya kukamatwa Babu Tale.soma zaid.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam
imetoa hati ya kukamatwa kwa Hamis Tale ‘Babu
Tale,’ ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa
bongo fleva, Diamond Platnumz, anaandika Faki
Sosi.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na
Babu Tale kutotii amri ya mahakama
iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh.
250 milioni.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana
na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe
Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za
mawaidha (DVDs ) bila ridhaa ya shekhe huyo,
jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale
kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa
tarehe 18, Februari mwaka huu, mahakama ilitoa
hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8
Julai mwaka huu.
Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza
Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi leo
tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata
wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza
kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya
mahakama.
Shauri hilo limetajwa tena leo mbele ya Juma
Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ametoa
hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi
Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.
Msajili Juma ametoa hati hiyo baada ya
Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde,
kuomba hati hiyo ipekwe Kinondoni kwa kuwa
Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala
kama hali ya kwanza ilivyoeleza.
Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine
Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200
milioni kama fidia ya kuvunja haki miliki ya
Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya
hasara aliyoipata kutokana na kuvunja
makubaliano.
Katika uamuzi wake Jaji Shangwa amesema, Juni
16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na
wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya
kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs
kwa ajili ya kuziuza nchini.
Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba,
kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia
walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na
kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye
ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake,
Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya
Hasara na Maadui wa Uislam.
Amesema, makubaliano ya awali yalikuwa
kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei
na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na
kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila
kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi
wake.
Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka
Mwaikugile na Clement Kihoko, alifungua kesi ya
madai namba 185/2013 akiiomba mahakama
iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama
fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni
kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na
kuvunjwa kwa makubaliano.chanzo mwanahalisioneline.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top