Watu 15 washilikiwa kwa tuhuma za uhalifu na unyan'ganyikwa kutumia silaha.soma zaid.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro,
Wilbrod Mutafungwa
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro,
linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za uhalifu na
unyang’anyi wa kutumia silaha, wakiwamo
wawili waliokuwa askari polisi.
Taarifa hiyo ilitolewa jana kwa vyombo vya
habari na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, watuhumiwa
hao walikamatwa na askari polisi kwa nyakati
tofauti katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
“Baada ya kuendesha msako, tulifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao, wakiwamo
wawili waliokuwa askari polisi zamani.
“Wale waliokuwa askari polisi, walifukuzwa kazi
baada ya kugundulika wanajihusisha na vitendo
vya ujambazi kwa kushirikiana na majambazi.
“Kwa ujumla, watuhumiwa hao pamoja na
kujihusisha na uhalifu, pia wanajihusisha na
biashara ya dawa za kulevya, ikiwamo bangi
bangi, cocaine na mirungi,” alisema Kamanda
Mutafungwa.
Aliwataja watuhumiwa waliokuwa askari kuwa ni
Elihuruma Mringi na Jakson Nzenzule, ambaye
inasemekana anatuhumiwa kumuua mwendesha
bodaboda aliyefahamika kwa jina la Nkassi
Massawe, mkazi wa Rombo, mkoani hapa.
Watuhumiwa wengine ni Maris Masamu (38),
Saidan Massawe (39), Godwin Mahenge (32),
Baraka Kimario (23) na Lightness Wilfred (29)
ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya
unyang’anyi wa kutumia silaha, kusuka mipango
ya uhalifu pamoja na mauaji.
Wengine ni Hilda Kihiyo (21), Elisayuni Eskael
(28), Rahel John (38), Sabina Rubei (30),
Elizabeth Mtui (33) na Zacharia Mlaki (22)
wanaotuhumiwa kuuza bangi na dawa nyingine
za kulevya.
Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa
alisema wamefanikiwa kuwakamata watu wawili
raia wa Kenya kwa tuhuma za utapeli
walioufanya katika Benki ya CRDB, Tawi la
Moshi mjini.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Edward
Kimata (53) na Chrispin Kanyuela (36), wakazi
wa Nairobi nchini Kenya.
0 comments :
Post a Comment