Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Soma sheria inayochanganua miamala ya biashara.soma zaid.


Sheria ya uuzaji wa bidhaa sura ya 214
ni sheria inayoeleza na kuchanganua
miamala ya biashara kwa ujumla
wake. Inaeleza mikataba ya biashara,
aina zake, watu wanaostahili kuingia
mikataba hiyo, biashara halali na
haramu, usafirishaji wa bidhaa
halikadhalika kupokea,kuharibika na
kupotea kwa bidhaa.
Kutokana na kukua kwa biashara na
kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa
hasa kutoka nje ya nchi au nje ya
mikoa kupitia mitandao au vinginevyo
makala yataeleza baadhi ya kanuni za
kisheria za kuagiza na kupokea mizigo
ambazo zitamsaidia mfanyabiashara na
hata mlaji.
1.HASARA NI YA NANI MZIGO
UKIPOTEA AU KUHARIBIWA WAKATI
WA KUSAFIRISHA.
Kifungu cha 34( 2 ) kinasema kuwa
ikiwa jukumu la kusafirisha mzigo/
bidhaa ni la muuzaji basi muuzaji
ndiye atakayetakiwa kuingia mkataba
wa usafirishaji mzigo kati yake na
msafirishaji(transporter).
Kifungu kinaendelea kusema kuwa ikiwa
mzigo utapotea wakati ukiwa njiani au
kuharibika kwa namna yoyote basi
muuzaji ndiye atakewajibika na
upotevu au uharibifu na mnunuzi
anaweza kukataaa kupokea mzigo
ulioharibika au akakubali kupokea lakini
akataka kulipwa fidia. Ikiwa umepotea
kabisa atahitaji kurudishiwa hela yake.
2.USIKUBALI KUPOKEA MZIGO/ BIDHAA
AMBAYO HAIJATIMIA .
Kifungu cha 32(1) cha Sheria ya uuzaji
bidhaa kinasema kuwa ikiwa muuzaji
atapeleka mzigo/bidhaa ambayo
haijatimia basi mnunuzi anaweza
kukataa kupokea mzigo huo.
Lakini ikiwa atakubali kupokea mzigo
huo ambao haujatimia basi atatakiwa
kulipa pesa ileile iliyo kwenye mkataba
bila kukata au kupunguza hela kufidia
bidhaa ambayo haijaletwa.
Kwahiyo ukikubali tu kupokea mzigo
ambao haujatimia huwezi tena kusema
napunguza na hela. Ukipokea tu sheria
inasema unatakiwa kulipia hela yote
mliyokuwa mmekubaliana. Hivyo basi
kama hauko tayari kulipa hela yote
basi lililo bora kwako ni kutopokea
kabisa mzigo huo.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

0 comments :

Post a Comment

Back To Top