Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Watuhumiwa wafikishwa polisi kwa kumfanyia unyama na kumtesa mtu mmoja mkoani Geita.soma zaid.

.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu
Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa
ziara ya kikazi kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za
mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china
wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna
uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua
ambao ni watanzania.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya
sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa
mitandaoni na kwenye vyombo vya habari
zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi
kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa
vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni
raia wa china.
Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama
wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya
ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa
taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa
watanzania.
Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo
na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo
mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza
fahamu na sio kifo.
Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda
gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo
kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa
kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.
Katika mahojiano ya waziri Mwigulu Nchemba na
kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo
aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa
uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na
mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati
yupo hapo gerezani.
Katika hali hiyo ilimlazimi Mh.Mwigulu kwenda
mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo
kwaajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo
vya kinyama.
Katika oparesheni hiyo, kijana aliyeteswa na
kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni
walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja
walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top