Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 27, 2016

Mahakama ya wilaya Mpanda imemkuta mh.Lawrence kego masha hana hatia.

Mahakama ya Wilaya, Mpanda imemkuta
Mh. Lawrence Kego Masha aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa
Nyamagana Mwanza pamoja na
washtakiwa wengi ambao ni Viongozi wa
Chadema Jimbo la Nsimbo, Katavi
kutokuwa na hatia katika makosa mawili
ya Kula Njama Ili Kutenda Kosa na
Kuhutubia Wakimbizi wakati wa Uchaguzi
Mkuu wa 2015 na kosa lingine la kuingia
makazi ya Wakimbizi bila Kibali.
Mahakama imesema kwamba upande wa
mwendesha mashtaka umeshindwa kutoa
ushahidi wowote unaonyesha kwamba
washtakiwa hao walikutana na kupanga
njama kutenda kosa. Pia hakuna ushahidi
wowote kuonyesha kwamba washtakiwa
walikamatwa wakihutubia wakimbizi.
Ila Mahakama iliona kwamba washtakiwa
hao wana kosa la kujibu kwa shtaka la
kuingia kwenye kambi/makazi ya
wakimbizi bila kibali. Mara baada ya
uamuzi huo washtakiwa walitakiwa kutoa
utetezi wao ambapo washtakiwa Lawrence
Masha na Stansalaus Kaswele walitoa
utetezi wakiongozwa na Wakili Albert
Msando.
Leo Mahakama imetoa hukumu na
kusema kwamba washtakiwa wote saba
hawana hatia kwa kukubaliana na hoja
zote za Wakili wa Utetezi. Hivyo
washtakiwa wako huru.
Chanzo: Wakili Msomi Albert Msando

0 comments :

Post a Comment

Back To Top