Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 13, 2016

Wazir mkuu wa uingereza amewaaga rasimi wabunge.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, leo
amefanya mkutano wake wa mwisho bungeni
baada ya kuhudumu kwa miaka 6.
Kulishuhudiwa malumbano makali kati yake na
kiongozi mkuu wa chama cha upinzani Labour,
Jeremy Corbyn, kuhusiana na uchumi na
migongano ya kungangania uongozi ndani ya
vyama vyote vya kisiasa.
Leo ni siku ya mwisho kwa Bwana David
Cameron kushikilia wadhifa wa waziri mkuu wa
Uingereza, baada ya kuhudumu kwa miaka 6.
Akiwa bungeni Cameron amejibu maswali ya
watunga sheria wa Uingereza na sasa
anatarajiwa kukutana na Malkia Elizabeth katika
ikulu ya Buckingham atakapowasilisha barua
yake ya kujiuzulu rasmi.
Uchangamfu wa vikao vya bunge la Uingereza
ulikuwepo kama kawaida lakini pia bw. Cameron
alibadilishana mawazo kuhusu maswala muhimu
ya kiuchumi na kiongozi wa chama kikuu cha
upinzani cha Leba ,Bw Jeremy Corbyn.
Wakati huo kiongozi mpya wa chama cha
Conservative Bi Theresa May alikuwa amekaa
karibu naye.
Cameron alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu
mwezi uliopita, baada ya kushindwa katika kura
ya maoni kuhusu uanachama wa Uingereza
katika muungano wa bara Ulaya EU.
Mrithi wake Bi May ameahidi kutekeleza uamuzi
wa Uingereza kujiondoa kutoka muungano wa EU,
licha ya yeye kupinga kauli kujiondoa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top