Aliyekuwa Msanii wa Taarabu Malehemu BI Shakila Said kuzikwa leo saa 10 alasir Mbagala jijini Dar.soma zaid
Kwa mujibu wa familia marehemu Bi.
Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo
Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri
katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko
Mbagala Charambe jijini Dar es salaam
Namna ya kufika msibani nyumbani kwa
marehemu kwa kutumia daladala.
Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu,
ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa
na unashuka Mnara wa Voda hapo
unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.
Bi Shakila alifariki jana baada ya
kuanguka nyumbani kwake mara baada ya
kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu
wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa
taarabu hakuwa anaumwa wakati mauti
yanamkuta.
KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI.
SHAKILA.chanzo michuzi blog
0 comments :
Post a Comment