Hakuna mwanamke anayependa kuolewa halafu kwa mda mfupi waachane.soma zaid
Hakuna mwanamke anayependa kuolewa na
mwanaume halafu kwa muda mfupi waachane,
bali kila mwanamke ana kiu ya kutaka kuishi na
ampendaye mpaka pale mauti yatakapo
watenganisha, Kwa misingi hiyo,ndoa ni jambo
muhimu na gumu kwa wakati mwingine hasa
linapokuja suala la kuchagua mwenzi wa kuishi
naye maishani, hivyo basi mwenye nia ya kuoa
utamtambua kwa haya.
ALIYE MKWELI.
Katika hili, hekima na busara nyingi huhitajika
kutumika, ngao kubwa ya utambuzi juu ya
mpenzi uliyenaye kuwa mume mwema
linategemea sana hili, Ukweli ni silaha muhimu
sana katika uhusiano, Japo natambua kuwa,
kuna wengine watajiuliza utajuaje kama huyu ni
mkweli au siyo. Kitendo cha kukutamkia kuwa,
anakupenda ni cha ukweli sana hasa kama
atakuwa anakupenda kwa dhati, Baadhi ya
wanaume wanafikia hatua kuongopa na hata
kuazima gari na kujifanya kuwa ni lake ili
akunase. Kumbuka wahenga walisema ‘njia ya
muongo ni fupi’ hivyo baada ya muda
utachambua pumba na nafaka.
ANAYEJALI
Wahenga waliendelea kunena,`nyota njema
huonekana alfajiri’. Huo ni msemo wa zamani
wa wazee wetu ambao una maana kubwa sana.
Kama mwanaume huyu ambaye kwa sasa ni
mchumba wako (wazazi wawe wanatambua)
anakupenda, lazima atakujali, kukuwazia wewe
katika maisha yake yote, hukuona kuwa wewe ni
mwenye thamani kubwa katika maisha yake,
Hatakusumbua kwa kutaka ngono kabla ya muda
muafaka wa kufanya hivyo. Anayejali afya yako
kwanza na hatathubutu kushiriki tendo la ndoa
kabla hamjapima virusi vya ukimwi,
anakupeleka hospitali unapokuwa mgonjwa
(haijalishi kama una wazazi au wasaidizi
wengine).
ALIYE NA MSIMAMO THABITI
Huyu huonekana mapema sana, asiyetingishika
wala kushawishiwa na marafiki zake, katika
mambo yasiyofaa, Hushikilia msimamo wake
katika kutekeleza yale yote aliyokuahidi na
aliyopanga kuyafanya kwa ajili
yenu, Mathalani, ameambiwa na watu kuwa
wewe una uhusiano na mwanaume mwingine,
Mwenye msimamo huchukua muda mwingi
kufanya uchunguzi juu ya aliyosikia kabla
hajakuuliza chochote.
Nathubutu kusema hivyo kwa sababu kuna
baadhi ya wanaume wana kasumba mbaya,
wanaposikia kitu kuhusu wachumba zao, au
wapenzi wao, kabla ya kufanya uchunguzi
humjia juu mwanamke husika na wakati
mwingine hufikia hata hatua ya kumpiga, Hii ni
hulka mbaya ambayo baadhi ya wanaume
wanayo, lakini jaribu kujiuliza, kama hamjaoana
anadiriki kukupiga kama ngoma na akikuoa je, si
atakufanya kilema?
ANAYESHAURIKA
Siku zote, amekuwa mkweli kwako,
anakubainishia mali zake pamoja na biashara
zake. Haoni vibaya pia kukufundisha juu ya
kuendesha mali zake. Inapotokea unamshauri,
hukusikiliza kwa makini na kufanyia kazi ushauri
unaompa. Mwanaume huyu hutulia na kuyapima
maneno yako kwa makini kabla hajayafanyia
kazi, Ni vyema mumeo ashaurike (inapobidi) ili
asifanye madhara mengine katika maamuzi ya
familia kwa kisingizio cha ubaba ndiyo kichwa
cha familia.
ANAYEJALI NDUGU ZAKO
Waswahili wanasema `ukipenda boga, penda na
ua lake’kwa wakati mmoja, msemo huu
unasisitiza upendo. Kwamba kuna vipimo
kadhaa vya upendo lakini moja ni kumwangalia
kama ana upendo na ndugu zako, Mwanaume
huyu mara zote hukuulizia hali ya wazee wako
pamoja na ndugu zako wengine. Hii ni sawa na
mawingu kabla ya mvua, Kwa sababu kama
atashindwa kuwajali ndugu zako japo kwa
kuwajulia hali utakapoingia katika ndoa
atakuruhusu ukawasabahi kweli? Hili ni kama
msingi katika kumpata mume bora.
0 comments :
Post a Comment