Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, August 20, 2016

Wazir mkuu ziarani katavi.soma zaid

MAPOKEZI makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili leo
mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya
siku nne mkoani Katavi inayoambatana na
kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya
maendeleo na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa
juu wa kitaifa kutembelea mkoa wa Katavi
tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia
madarakani, ziara ambayo itamfikisha pia katika
mkoa jirani wa Rukwa.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi,
Lauteli Kanoni amesema ziara ya Waziri Mkuu
mkoani humo itaanza leo na kutarajiwa
kuhitimisha ziara yake Agosti 23, mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba, Waziri Mkuu atawasili leo
mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Mpanda
kisha ataelekea Ikulu Ndogo ambako
atasomewa taarifa ya mkoa na kuzungumza na
watumishi wa serikali katika viwanja vya ikulu
ndogo.
Siku itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha
Majalila, kunakojengwa Ofisi za Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji
kijijini humo kabla ya kuhutubia mkutano wa
hadhara.
Kwa mujibu wa ratiba yake, anatarajiwa
kuhutubia mikutano ya hadhara katika kijiji cha
Ndui kilichopo kwenye makazi ya wakimbizi ya
Katumba na katika uwanja wa Azimio, Manispaa
ya Mpanda.
Aidha, Agosti 22, mwaka huu Waziri Mkuu
atafanya ziara ya siku moja katika wilaya ya
Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa
Inyonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
kabla ya kuelekea katika Kijiji cha Majimoto,
Halmashauri ya Mpimbwe atakapokagua ujenzi
wa daraja la mto Kavuu na baadaye kuhutubia
mkutano wa hadhara.
Waziri Mkuu Majaliwa anatarajiwa kufanya
majumuisho ya ziara yake Agosti 23, mwaka
huu katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini
Mpanda kabla ya kuelekea wilayani Nkasi
kuanza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top