Msanii wa nyimbo za Taarabu Khadija Said afariki dunia.soma zaid
Habari za kusikitisha zimetufikia muda
huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi.
Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo
muda mfupi baada ya kuanguka na
kukimbizwa hospitali ya karibu na
nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini
Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la
Muziki Tanzania Bw. Addo November, Bi
Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya
kumaliza kuswali alianguka ghafla na
alipofikishwa hospitali alikokimbizwa
alikutwa amekwishafariki. Taarifa kamili
ya mipango ya mazishi
tutawaletea mara tu tutapozipata.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA
MAREHEMU - AMINA
Bi Shakila enzi za uhai wake takriban
miezi sita iliyopita.
0 comments :
Post a Comment