Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, August 20, 2016

Vigogo wawili NIDA wapata dhamana.soma zaid

VIGOGO wawili wa Mamlaka ya Vitambulisho
(NIDA) wanaokabiliwa na mashitaka ya
kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.2
wameachiwa kwa dhamana.
Washitakiwa hao ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Biashara, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.
Hata hivyo, washitakiwa wengine akiwemo
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
hiyo, Dickson Maimu na wenzake watano
wanaendelea kusota rumande.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Respicius Mwijage alitoa uamuzi
huo jana kwa kuwa washitakiwa hao wawili
hawaguswi katika mashitaka yaliyofunguliwa
chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Alisema anakubaliana na hoja za upande wa
utetezi zilizowasilishwa na Wakili Johnson
Jamhuri kuwa mashitaka yanayowakabili
washitakiwa hao yana dhamana na hayahitaji
kuombewa dhamana hiyo Mahakama Kuu.
Hakimu Mwijage alisema, washitakiwa
wanatakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini
wawili ambao watasaini hati ya Sh mil 200, pia
wawasilishe hati zao za kusafiria na
hawatakiwa kwenda nje ya Dar es Salaam bila
kibali cha mahakama.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top