Sumatra wasema hakuna mgomo wa mabasi jumatatu.soma zaid.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra) imewatoa hofu Watanzania kuhusu
taarifa za kutokuwepo kwa huduma ya usafiri
wa mabasi kwenda mikoani kuanzia Jumatatu
na kusema kuwa inafuatilia kuhakikisha kuwa
huduma hiyo inatolewa wakati wote.
Pia, imesema maazimio yaliyotolewa na Chama
cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) kuhusu
kufanyika kwa ukaguzi wa mabasi yote
yaendayo mikoani Agosti 22, mwaka huu,
usitishwe na kuwataka kutoa huduma hiyo hadi
utaratibu maalumu utakapopatikana.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi
Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe, alisema
Taboa ilipeleka maazimio matatu yanayohusu
ukaguzi wa magari unaolenga kuimarisha
usalama na ubora wa huduma wanazotoa kwa
jamii.
Ngewe alisema mamlaka hiyo inakamilisha
utaratibu huo wa kukagua magari pamoja na
madereva na kwamba wanahitaji kuzungumza
na taasisi inazoshiikiana nazo, ikwemo Kikosi
cha Usalama Barabarani.
“Maazimio haya ni mazuri na yanalenga kutoa
huduma bora lakini hatuwezi kuanza ukaguzi
Agosti 22 kwa kuwa tunahitaji vifaa kwa ajili ya
kufanya ukaguzi huo na kujua ni mabasi yapi
yataanza ukaguzi na yatakayofuata,’’ alisema
Ngewe na kuongeza kuwa, wamiliki wa mabasi
hayo pamoja na madereva wanatakiwa kufuata
masharti ya leseni walizopewa kwa kusafirisha
abiria hadi utaratibu rasmi wa ukaguzi
utakapotolewa.
Hata hivyo, alisema wananchi hawana budi
kuondoa hofu ya kukosa usafiri kwakuwa hakuta
utakaositishwa ili kupisha ukaguzi huo.chanzo muungwana.com
0 comments :
Post a Comment