Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, August 16, 2016

Donalf Trump aendelea na msimamo wake wa kupambana na Ugaid.soma zaid

Mgombea urais wa Marekani kwa kupitia tiketi
ya Republican, Donald Trump anaonekana
kuendeleza vimbwanga kila ku kicha, katika
kampeni zake za kuwania kiti cha urais nchini
humo.
Trump ambae amekua akiwaomba wamarekani
kumpa kura ili aweze kurudisha hadhi ya nchi
hiyo kwa kuimarisha hali ya kiuchumi na
kuiweka katika hali salama kwa kupambana na
ugaidi wa waislamu wenye itikadi kali.
Amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa
Marekani atabadilisha sera za mambo ya nje ya
nchi hiyo yenye lengo la kujenga taifa kwa kuwa
na sera zanye uhalisia.
Akihutubia mkutano wake katika jimbo la Ohio,
mgombea huyo alisisitiza juu ya umuhimu wa
mpango wa muda wa kuzuia viza za waombaji
wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya
kueneza ugaidi na kupendekeza kuanzishwa kwa
mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na
uchunguzi wa akaunti zao za mitandao ya
kijamii.
Aidha Trump ameonesha nia ya kuwa tayari
katika kushirikiana katika kazi na nchi yeyote ile
bila kujali tofauti za kiitikadi lakini akiwa na nia
ya kusaidia kulitokomeza kundi la Islamic State
(IS).
Chanzo: BBC Swahili

0 comments :

Post a Comment

Back To Top