Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, August 16, 2016

Wanachama wa Yanga wamemtolea uvivu Akilimali Yahaya.soma zaid

Kufuatia tetesi za Mwenyekiti wa Yanga Yusuph
Manji kubadili msimamo wake wa kuikodi timu
hiyo, wanachama wa klabu ya Yanga Kanda ya
Dar es Salaam wamempigia magoti na kumsihi
asibadili maamuzi yake.
Wanachama hao wamemuomba Manji kutobadili
msimamo wake leo katika kikao cha dharula
kilichoketi leo kwenye makao Makuu ya timu
hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha wanachama hao wameikemea tabia ya
baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuzungumza na
vyombo vya habari pasipo kupata ridhaa ya
chama.
Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Kanda ya Dar
es Salaam, Robert Lyungu Kasera amemtaka
katibu wa timu hiyo Taifa kumfuta uanachama
Katibu wa Baraza la wazee la Yanga Taifa,
Ibrahim Akilimali kwa madai kuwa kiongozi huyo
anashirikiana na timu pinzani kukwamisha
mpango wa Manji kuikodi timu.
“Akilimali anashirikiana na Simba kuiharibu
Yanga hatufahi, haiwezekane aongelee masuala
ya Yanga pasipo ridhaa ya uongozi wa klabu, ”
amesema Lyungu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top