Godbess Lema na Dc Mrisho Gambo hapatoshi waendelea kuvutana.soma zaid
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema
(Chadema) ameendelea kuvutana na Mkuu wa
Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo, baada ya
kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Lema ameiomba ofisi ya Katibu Tawala wa
Mkoa wa Arusha (RAS) kumsimamia na
kumuonya mkuu huyo wa wilaya kwa kile
alichosema anaingilia shughuli za halmashauri
ya Jiji la Arusha.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipozungumza
na waandishi wa habari.
Msimamo huo wa Lema ni mwendelezo wa
kutoelewana na mkuu huyo wa wilaya kwa kuwa
hivi karibuni walichongeana mbele ya Naibu
Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo, alipofanya
ziara mkoani hapa.
Katika maelezo yake jana kwa waandishi wa
habari, Lema alisema Gambo anaingilia
majukumu ya halmashauri na kwamba tabia
hiyo inarudisha nyuma utendaji wa madiwani wa
halmashauri hiyo.
“DC amekuja na kiherehere sana, yaani
anaingilia shughuli za halmashauri wakati akijua
chama chake hapa kina diwani mmoja.
0 comments :
Post a Comment