Eneo la ikulu ndogo mbeya limemegwa na kuuzwa.soma zaid
ENEO lililokuwa limetengwa ili ijengwe Ikulu
ndogo ya Mkoa wa Mbeya limemegwa na
kuuzwa. Limeuzwa kutokana na kile
kinachotajwa kuwa ni maofisa wa ardhi Jiji la
Mbeya, kutumia fursa ya eneo hilo kujinufaisha
kwa kuuza viwanja.
Inaelezwa kuwa baadhi ya maofisa ardhi wa
halmashauri ya jiji, wamepima viwanja kwenye
eneo hilo wakishirikiana na wakazi ambao
ilikuwa walipwe fidia kwa mashamba yao, na
wakazi hao wanatumiwa kutafuta wateja wa
viwanja hivyo ili ionekane wao ndiyo walioviuza
kwa watu wanaojenga sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla jana
alitembelea eneo hilo lililopo Veta jijini Mbeya
na kujionea majengo yaliyojengwa kwenye ardhi,
iliyokuwa sehemu ya uwanja wa kujengwa Ikulu
ndogo ya Mkoa.
Diwani wa Kata ya Ilomba, Dickson Mwakilasa
alimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa eneo
lilikojengwa nyumba za watu binafsi, lilikuwa la
serikali na kilichotakiwa ni kulipa fidia kwa
wakazi waliokuwa na mashamba maeneo ya
jirani.
Kufuatia hali hiyo, Makalla alilazimika kuwahoji
maofisa wa halmashauri ya jiji, lakini wote
wakaonekana kutoijua vyema historia ya eneo
hilo, hivyo ikamlazimu Mkuu huyo wa Mkoa
kuahidi kufuatilia kwa haraka nyaraka husika.
Alisema anachotaka kujua ni ramani
inayoonesha ukubwa wa eneo la awali; na pia
matumizi yaliyopangwa, huku akisema
anachojua yeye mpaka sasa ni kuwa maofisa
ardhi wameuza kinyemela sehemu ya uwanja
wa Ikulu ya Mkoa.
0 comments :
Post a Comment