Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 31, 2016

Kamati ya Bunge imeibana Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi(HLSB).soma zaid


Kamati ya Bunge yaibana Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi
Wabunge wameibana Bodi ya Mikopo kwa
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa
kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni
katika kipindi kifupi kiasi ambacho hakilingani na
kazi wanayoifanya.
Kwa kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa
lawama kwa kuchelewesha mikopo, kushindwa
kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na
kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa.
Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema
bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo
kwa vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa
1,000.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB,
Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele ya kamati
hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na
kwamba wanaweka mikakati mizuri ya
kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha
inafanya kazi kwa weledi zaidi.
Wakizungumza katika kikao cha Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha
kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha
2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao
walisikitishwa na kitendo cha bodi hiyo
kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni
walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu
ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu.
Walisema isipobadilika katika utendaji wake,
kuna haja ya Serikali kuivunja na kuchagua
benki moja kusimamia shughuli hiyo.
“Mnatakiwa kuongeza juhudi na mikakati ili
kuhakikisha kwamba madeni yote yanakusanywa
kwa wakati la sivyo naona kuna haja ya Serikali
kuivunja bodi nakutafuta njia nyingine,” alisema
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Raisa Mussa.
Mbunge wa Same Mashariki (Chadema),
Naghenjwa Kaboyoka alihoji kwa nini pamoja na
bodi hiyo kuwa na mameneja 18 na wafanyakazi
wa kudumu 144, bado utendaji wao umekuwa
siyo wakuridhisha.
“Kwa idadi yenu tulitegemea kupata ripoti
inayojitosheleza na hata utendaji wenu ulitakiwa
kuwa wa ufanisi zaidi,” alisema.
Akijitetea zaidi, Badru alisema kuna
changamoto nyingi zinazoikabili bodi yake lakini
kwa sasa wamepiga hatua kubwa katika
ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika
wa mfuko huo.
“Kwa mfano Mei mwaka huu tulikusanya kiasi cha
Sh2 bilioni na Juni tulikusanya Sh6 bilioni,”
alisema.
Aliongeza kuwa ipo mikakati mingi ambayo
wamejiwekea katika kuhakikisha kwamba bodi
hiyo inakusanya madeni kikamilifu kutoka kwa
wadeni wake wote.
“Kwa kupitia mikakati yetu, tumeweza kuongeza
idadi ya wanafunzi ambao tunawapa mikopo
kutoka 42,729 hadi 123,783. Katika kipindi hicho
fedha za mikopo zimeongezeka kutoka Sh56
bilioni hadi kufikia Sh465.3 bilioni,” alisema.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top