Halmashauli ya moshi imetenga asilimia 10 kuwakopesha wanawake na vijana wajasiliamali.soma zaid
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa
Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya
Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto)
alipomtembelea ofisini kwake na kufanya
mazungumzo nae akiwa ameambata na
Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la
Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa
Angela Kizigha.
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya
Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto)
akizungumza na Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Mh.Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa
Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa
Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada
ya mazungumzo yao.
Na Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
ameendelea na ziara yake ya
kujitambulisha kwa viongozi wa dini
ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa
kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa
kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Mchungaji Solomon
Masangwa , Askofu wa Kanisa la
Evangelistic Assemblies of God(EAGT)
mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na
Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la
Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na viongozi hao kwa
nyakati tofauti mbali na kujitambulisha
aliwahakikisha dhamira ya serikali
kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya
kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa
muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa
la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John
Joseph Magufuli kutaka kuwainua
wananchi wa chini kupitia mapato ya
ndani halmashauri zimetenga asilimia 10
kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya
mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake
na Vijana wajasiriamali
zitakazowawezesha kufanya shughuli za
uzalishaji mali.
Amewataka wawajulishe waumini wa dini
zote na serikali iko tayari kupanga
utaratibu wa
maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana
kupita na kutoa elimu kwa makundi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu
ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika
mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala
kisiasa.
Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi
wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na
kuomba vyombo vya ulinzi na usalama
ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti
wake kukabiliana na changamoto za
kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa
amani.
Aidha alishauri kutokana na idadi ya
watu wanaotumia usafiri wa anga
kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria
uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa
ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili uweze
kukidhi mahitaji ya sasa badala ya
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao
kuwa serikali itakua ikiwashirikisha
mipango mbalimbali inayokusudia
kuitekeleza ili watoe mawazo yao katika
kuiboresha na kuifanya itekelezeke kwa
wepesi zaidi.
0 comments :
Post a Comment